• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Tabora Vijijini
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

CWT YATAKA WATENDAJI WAJALI HAKI ZA WATUMISHI

Posted on: January 14th, 2019

CWT YATAKA WATENDAJI WAJALI HAKI ZA WATUMISHI

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Leah Ulaya  amewaomba Watendaji Wakuu wa Halmashauri ya Manispaa , Wilaya na Mji mkoani Tabora kuhakikisha wanajali haki za watumishi waliochini yao ambazo zipo ndani ya uwezo wao ili kuondoa manung’uniko yanayoepukika.

Hatua hiyo itasaidia kuendeleza mshikamano na ushirikiano baina ya watumishi na Serikali na kufanya kuwepo na utendaji wa pamoja.

Ulaya alitoa ombi hilo jana Mkoani Tabora wakati wa mkutano wa wadau wa elimu mkoani humo uliolenga kuimarisha ushirikiano na uhusiano kati ya walimu , Serikali na CWT.

Alisema mambo mengine yanayodaiwa na watumishi wakiwemo Walimu yako ndani viongozi kama vile Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Maafisa Utumishi  na Maafisa Elimu wala hayaitaji viongozi wa Wizara ndio mtumishi apate haki yake.

“Nitoe ombi langu kwa viongozi wa wetu wa mkoa wa Tabora Maafisa utumishi , Maafisa Elimu na wengine wote tuhakikishe kwamba tunajali haki za watumishi wetu  husasani ni walimu yapo mambo ya kawaida ambayo yapo chini yenu kama Mkurugenzi” alisema.

“Masuala kama nauli ya likizo ni nyinyi wenye huku na mambo mengine…tuendelee kuwaomba kwa sababu mshikamano huu tuhakikishe kwamba tunaendelea kutimiza wajibu wetu kwa kadiri tutakavyoweza” alisisitiza.

Aidha Ulaya alisema mwelekeo wa CWT ni kuhakikisha inasimimia wajibu wa Mwalimu kufanyakazi zake kwa ufanisi kwa sababu inaamini kuwa bila ya kutumiza wajibu walimu hawatakuwa na haki ya kudai kile wanachostahili kudai.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey  Mwanri aliwataka Wakurugenzi Watendaji  na wale Maofisa wanaoshughulikia masuala ya utumishi wanapowapandisha madaraja watumishi wakiwemo walimu wahakikishe wanabadilisha na mishahara yao na sio kubaki na ile ya   cheo cha zamani.

Aliongeza kuwa wanawahamisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine pia wanapaswa kuwalipa stahili zao kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya utumishi wa umma inavyotaka kabla hajaondoka katika kituo chake za zamani kuelekea kipya.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema kama Halmashauri zitakuwa hazina fedha katika kipindi mwalimu au mtumishi anadai ni vema wakaweka utaratibu kuwaandikia barua mtumishi la kutambua deni lake  ambalo limeshaidhinishwa ofisi ya Mkaguzi wa Ndani kwamba ni halali ili hata kama ikitokea  bahati mbaya akapata tatizo ndugu zake  wawe na msingi wa kudai.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Tabora Hamis Lissu alisema wamekutatana kwa lengo kujenga desturi ya uwajibikaji wa pamoja katika kufikia malengo yaliyokusudiwa ya utoaji elimu bora katika Mkoa wa Tabora.

Aliongeza  kuwa wamekutata ili kuondoa tofauti ndogo ndogo miongoni mwao ili kuwa na mwelekeo wa pamoja katika kuendeleza elimu kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo nchini.

Mwisho



Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2018 January 24, 2019
  • TELEPHONE DIRECTORY October 16, 2018
  • WATEULE July 30, 2018
  • AJIRA MPYA ZA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI, JULAI, 2018 July 18, 2018
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAHAKAMA MKOANI TABORA YATAKIWA KUANZISHA MAHAKAMA ZINAZOTEMBEA

    February 06, 2019
  • RAS TABORA AAGIZA WAKUU WA IDARA KUTOA MAFUNZO KUHUSU HAKI ZA BINADAMU KWA WALIOCHINI YAO

    January 01, 2019
  • WAKULIMA KUSAJILIWA NA KUPATIWA VITAMBULISHO NCHINI

    January 18, 2019
  • WADAU WAKUTANA TABORA KUANDAA JUMBE ZA KUTOKEMEZA UKATILI WA WANAWAKE NA WATOTO

    January 14, 2019
  • Angalia zote

Video

JPM BANDARINI
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • Government Portal
  • Sekretarieti ya ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile: 0786222266

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

Waliotembelea

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa