JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
USHIRIKA
 
Ushirika [ Nyumbani ] au
 
 
 

SEKTA YA USHIRIKA:

 

Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS):

Mkoa unazo jumla ya SACCOS 217 zenye wanachama 16,998 wakiwa na mtaji wa Shs. 374,413,313/=.

SACCOS za Mkoa wa Tabora zilipata mikopo ya jumla ya Shs.4,935,885,000/= toka taasisi zinazokopesha fedha, CRDB Shs.4,685,885,000/= na SCCUL TShs.250,000,000/=. Kiwango cha marejesho mikopo kimeongezeka toka marejesho ya awali ya tshs.483,600,000/= (asilimia 10.5) mwaka 2007 mpaka kufikia Tshs.2,579,715,000/= (asilimia 52.2) hadi Juni, 2010. (Ongezeko la asilimia 40.7)

 

MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA USHIRIKA:

•  Wananchi wengi wamehamasika na wamejiunga na Vyama vya Ushirika. Aidha, Vyama vya Ushirika 68 vya aina mbalimbali vimeandikishwa katika kipindi cha mwaka 2008/09 na 2009/10 kutokana na hamasa hiyo.

•  Kuhamasisha kuanzisha Benki ya Ushirika ya Mkoa.

 

CHANGAMOTO ZINAZOVIKABILI VYAMA VYA USHIRIKA:

•  Wanachama wa SACCOS hawazingatii masharti ya mikopo kutokana na uelewa mdogo kuendeleza Vyama vya Akiba na Mikopo.

•  Bei ndogo ya mazao ya biashara.

•  Vyama vya Ushirika kushindwa kustahimili ushindani katika mfumo wa Soko huru.

•  Bado kuna tatizo la kutorosha tumbaku kutoka chama kimoja cha ushirika hadi kingine kwa lengo la kukwepa urejeshaji wa madeni ya pembejeo.

•  Vyama vya Ushirika kuwa na mitaji midogo kutokana na kila kijiji kutaka kuwa na Chama cha Ushirika.

•  Vyama vya Ushirika kutokuwa na uongozi imara.

•  Wanachama wa Vyama vya Ushirika kugombea madaraka na kusababisha kubadili uongozi mara kwa mara.

•  Wanachama kupoteza imani kwa vyama vyao vya Ushirika kwa kushindwa kukidhi mahitaji yao.

•  Kutokuwa na uwazi katika uendeshaji wa shughuli za vyama vya ushirika.

•  Viongozi na watendaji kujilimbikizia mamlaka ya maamuzi hivyo kuonekana ndio wamiliki wa Chama cha Ushirika.

 

MIKAKATI YA KUKABILI CHANGAMOTO:

Katika kuzikabili changamoto hizo hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na:

•  Kuanzisha Benki ya Ushirika ya Mkoa ambayo itatoa mikopo kwa ajili ya pembejeo.

•  Kuimarisha SACCOS ziweze kutoa mikopo kwa wanachama wake ili waweze kujitafutia pembejeo.

•  Kuanzisha mfumo wa Stakabadhi ya Mazao Ghalani ili kusaidia kutafuta bei nzuri kwa mazao ya wakulima.

•  Kuendelea kutoa elimu kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika kuhusu kuimarisha vyama vyao kwa kuchagua viongozi bora, kwa kujaza fomu maalum ambayo inaeleza sifa ya kiongozi wa Chama cha Ushirika.

•  Kuwachukulia hatua za kisheria wanachama/wakulima wanaokiuka taratibu na kanuni za zao la tumbaku.

•  Kuendelea kuwahamasisha wananchi kuanzisha na kuimarisha Vyama vya Ushirika.

•  Kutoa elimu kwa wanachama ili waelewe kuwa chama ni mali yao, hivyo wana wajibu wa kusimamia uendeshaji wa shughuli zake na wao kutimiza wajibu wa uanachama na kuhoji mambo yanayofanyika kinyume na taratibu za uendeshaji wa vyama vya ushirika.

•  Kubandika kwenye mbao za matangazo taarifa mbalimbali ikiwemo Taarifa ya fedha.

Soma zaidi kuhusu mada >>

 
         
 
Ushirika [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, S.L.P. 25, TABORA. TEL: 026 - 2604058/2604116, FAX: 026-2604274