JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
TEKNOHAMA
 
Teknohama [ Nyumbani ] au
 

SEKTA YA NISHATI:

NISHATI:

Katika Mkoa wa Tabora Wilaya zote 6 zimeunganishwa na umeme wa Grid ya Taifa.

Mkoa una vituo 2 vinavyopokea umeme wa Grid ya Taifa navyo ni:

•  Kituo cha Tabora Mjini

•  Kituo cha Lusu Wilaya ya Nzega.

 

Kituo cha Tabora Mjini kina Transformer 2 kubwa za MVA 15 kila moja na matumizi ya juu ?maximum Demand" ni 10 MVA kwa mwezi.

Kituo cha LUSU-NZEGA Kina Transformer 1 kubwa yenye MVA 15 na ina matumizi ya juu ‘‘maximum Demand'' 10 MVA kwa mwezi.

Mpaka sasa wateja wa majumbani wapatao 16,005 wanapata huduma ya umeme, pia viwanda 3 vimeunganishwa na huduma hii. Aidha huduma ya umeme inapatikana katika Vijiji 24 kati ya Vijiji 488 vilivyoko Mkoani.

Miji midogo/vituo vya biashara vilivyo kwishafikishiwa nishati ya umeme wa Grid ya Taifa ni Makao Makuu ya Wilaya zote, isipokuwa Uyui. Vituo vya Biashara vilivyokwisha fikishiwa huduma ya umeme ni Kaliua, Usoke, Tutuo, Nata na Nzega ndogo.

 

i) Kupeleka Umeme wa Grid katika Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui

Urefu wa 'line' hii ni kilometa 44 toka Tabora Mjini na katika mradi huu Vijiji vitakavyo nufaika kwa kupata umeme ni pamoja na Manoleo, Mayombo, Magiri, Ilalwansimba, Isikizya na Idete. Jumla ya gharama za mradi huu ni Tshs. 2.1 bilioni. Hadi sasa njia hii ya umeme imekwishawekewa waya kutokea kituo kikuu cha umeme cha mjini Tabora, Isikizya Makao Makuu ya Wilaya.

ii) Kupeleka Umeme Katika Makao Makuu ya Tarafa ya Bukene

Wilayani Nzega .

Urefu wa 'line' hii ni kilometa 40 toka Nzega mjini. Katika mradi huu vijiji vitakavyonufaika na huduma ya umeme ni pamoja na Ijanija, Itobo, Busasi, Nawa na Kituo cha Biashara cha Bukene. Jumla ya gharama za mradi huu ni Tshs.2.1 billioni. Zabuni ya kupima njia hii ya umeme imekwishapitishwa.

 

SEKTA YA MAWASILIANO:

 

Mawasiliano ya Mkoa wa Tabora yanategemea barabara, viwanja vya ndege/anga, njia ya reli, simu, huduma ya Posta na simu za upepo "radio call".

VIWANJA VYA NDEGE:

Mkoa una jumla ya viwanja vya ndege kumi na tano (15). Kiwanja kikubwa kiko Tabora Mjini ambacho kina uwezo wa kuhudumia

ndege zenye ukubwa wa kubeba watu hadi 50. Mashirika ya ndege yanayotua kwenye kiwanja cha Tabora Mjini ni Precision na Air Tanzania Corporation (ATC). Ndege ndogo za kukodi pia hutumia kiwanja cha Ndege cha Mjini Tabora.

Viwanja vilivyoko Wilayani (14) ni kwa ajili ya huduma ndogo ndogo mfano, Madaktari watoa Huduma ya Haraka"flying doctors" na kunyunyizia dawa ya kuua nzige na ndege waharibifu (quelea quelea).

Kiwanja cha ndege cha Tabora kina barabara (runways) mbili zinazotumiwa na Ndege kutua na kuruka zenye urefu na upana kama ifuatavyo:

•  'Runway' 13/31 ina urefu wa meta 1,786 na upana wa meta 46.

•  Runway 08/26 ina urefu wa meta 1,555 na upana wa meta 30.

Runway zote 2 zimetengenezwa kwa changarawe isipokuwa meta 400 mbazo ni "concrete slabs". Aidha, kiwanja hiki kinatumika kwa ndege zote zisizozidi uzito wa kilo 51,600 na kinatoa huduma za Zimamoto kwa kiwango cha “Category “3” kulingana na viwango vya Shirika la Kimataifa la Usalama wa Anga (ICAO).

 

•  Ukarabati wa Barabara za Kurukia Ndege:

Mkoa wa Tabora unaishukuru Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania ambayo katika mwaka wa fedha 2007/2008 iliwezesha kufanyika matengenezo katika uwanja huo kwenye njia ya kurukia ndege yaliyojumuisha kufukia mashimo katika baadhi ya maeneo na pia kukwangua na kujenga tabaka lililoimarishwa kwa saruji katika njia Kuu ya kurukia ndege 13/31. Matengenezo hayo yaligharimu jumla ya Tshs. 70.0 milion.

Katika mwaka wa fedha 2008/2009 Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ilitumia Tshs. 65.0 million kwa ajili ya matengenezo madogo madogo katika kiwanja hiki na kuendelea kufanyia kiwanja hiki usanifu wa kina kwa udhamini wa Benki ya Dunia ili kiweze kujengwa kwa kiwango cha Lami. Usanifu wa kina kwa ajili ya matengenezo kwa kiwango cha lami umekamilika.

 

b) Changamoto Zinazohusu Kiwanja cha Ndege cha Tabora:

Njia za kurukia na kutua Ndege zimechakaa kutokana na umri mkubwa hivyo unahitajika ukarabati mkubwa.

Uwanja huu hauna uzio, hivyo watu na mifugo hukatisha kwenye uwanja ambapo ni hatari kwa usalama wa wananchi na mifugo.

 

c) Mikakati:

Kutokana na hali hii, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege imepanga kujenga uzio wa uwanja huo kwa awamu kwa kadri fedha zitakavyokuwa zikipatikana


RELI:

Mkoa wa Tabora unapata huduma ya reli ya kati kwa urefu wa km.794 ambayo inatoa mchango mkubwa kwa uchumi wa Mkoa kwa kusafirisha abiria, mbolea, mizigo na mazao mbalimbali.

Mpango Kazi (Business Plan) ya Kampuni ya Reli (TRL) kwa Mwaka 2008/2009 ulihusisha shughuli zifuatazo:

•  Kuongeza idadi ya safari za treni za abiria kufikia angalau safari sita kwa wiki - (safari za kutoka DSM/ TBR na TBR/DSM)

•  Kuongeza idadi ya mabehewa ya mizigo ya aina zote

•  Kuongeza idadi ya Engine (Locomotive)

•  Kuimarisha ulinzi na usalama wa abiria na mizigo yao

•  Kuimarisha mtandao wa reli na mawasiliano .

Hata hivyo hadi mwezi Juni 2009 mpango kazi huo haukutekelezwa kutokana na kukosekana fedha.

 

SIMU:

Huduma za simu za kawaida hutolewa na TTCL katika miji yote ya Makao Makuu ya Wilaya na ya Mkoa wa Tabora. Huduma hizo ni pamoja na zile zinazotumia nyaya na zisizotumia nyaya (CDMA).

 

Simu za Mkononi:

Makampuni manne VODACOM, TIGO, ZAIN na Zantel yanatoa huduma ya simu za mkononi kwa Miji ya Wilaya zote Mkoani Tabora. Karibu robo tatu ya Vijiji vya Mkoa wa Tabora hupata huduma za simu za mkononi.

Kampuni ya VODACOM na ZAIN mbali na shughuli ya mawasiliano hutoa huduma ya kutuma fedha -'M Pesa' na ‘ZAP'.

 

POSTA:

Mkoa una jumla ya Posta kubwa 5 na Posta ndogo 10. Huduma za Posta hutolewa kwenye kila Mji Mkuu wa Wilaya. Hata hivyo huduma za kusafirisha barua zimepungua sana baada ya kuanzishwa huduma za simu za mkononi.

Mpango Kazi (Business Plan) Kwa Mwaka 2008/09 ulikuwa na shughuli zifuatazo:

•  Uanzishaji wa "Internet Cafes": Shirika linatarajia kuanzisha huduma ya “Internet Café” katika Posta ya Nzega, Igunga, Urambo na Sikonge. Kwa sasa huduma hii inapatikana katika Ofisi Kuu ya Mkoa.

•  Uanzishwaji wa “Electronic Money Transfer/Counter Automation:

Ofisi Kuu ya Posta ya Mkoa, inategemewa kuunganishwa katika mtandao wa usafirishaji wa fedha kupitia “Computer badala ya utumaji kupitia katika 'Fax Machines' kama ilivyo sasa ifikapo mwaka 2009.

 

(c) Kukuza/Kupandisha Daraja Baadhi ya Ofisi za Posta:

Ofisi za Wakala zifuatazo zinategemewa kupewa hadhi na kuwa Ofisi:

•  Nkinga Franchised Post Office - Ndani ya Wilaya ya Igunga.

•  Ndala Franchised Post - Ndani ya Wilaya ya Nzega

(d) Mikakati ya Kuongeza Huduma ya Biashara na Tija :

 

i. Biashara ya barua:

Kuboresha usafirishaji wa mifuko ya barua kwa kutafuta na kuongeza Wakala wa usafirishaji wenye vyombo vya usafiri.

 

ii. Matangazo:

•  Kufanya matangazo ya biashara Mijini na Vijijini kupitia vipeperushi na "Loud Speaker? ili wateja waweze kuzifahamu na kuzitumia.

•  Kutafuta bidhaa za kutosha za maduka "Post Shops? zinazouzika kwa haraka, kuzitangaza na kuzitafutia soko.

Hata hivyo, mikakati na mpango kazi huo havikutekelezwa kutokana na kukosekana fedha

SIMU ZA UPEPO:

Mkoa una jumla ya Simu za Upepo (Radio Call) 66 ambazo hutumika sana kwenye Vituo vya Afya vilivyo mbali na Makao Makuu ya Wilaya, kwenye hospitali, Idara za Kilimo na Vituo vya Polisi.

INTERNET:

Huduma ya Internet (Internet Cafes) hupatikana katika miji ya Tabora, Nzega na Urambo. Hata hivyo huduma hiyo imesambaa sana kwenye Taasisi mbali mbali za Serikali na zisizo za Serikali. Aidha huduma ya Internet iko pia kwa watu binafsi.

RADIO:

Wakazi wa Mkoa wa Tabora husikiliza radio mbali mbali za ndani (Local Radio) na za nje kama ifuavyo:-

•  Radio za Ndani: TBC, Radio Free Africa (RFA)

•  Radio za Nje: Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Radio Ujerumani, Radio Peking n.k.

•  Pia kuna radio za ndani ya Mkoa (Local Radio) ambazo ni VOT FM na CG FM. Radio zote hizo husikika vizuri.

TELEVISION (TV):

Kwa walio na TV hutumia moja wapo ya njia zifuatazo ili waweze kuona vipindi vya TV, nazo ni:

•  Kufunga Dish. Njia hii imeenea sana hadi Vijijini.

•  Kufunga Antenna.

•  Kuvuta Cable. Huduma hii imeenea hasa kwenye miji ya Tabora (kuna Tabora Television – TTV na California).

•  TV nyingi zina uwezo wa kuona matangazo yanayorushwa na TBC, Star TV, ITV, Channel 5, Channel 10, BBC, CNN, Channel za nchi jirani kama vile Uganda na Kenya.

 

Soma zaidi kuhusu mada >>

 

 
         
 
Teknohama [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, S.L.P. 25, TABORA. TEL: 026 - 2604058/2604116, FAX: 026-2604274