|
||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||
MABORESHO YA UTUMISHI WA UMMA KATIKA MKOA:
Mkoa umeendelea kusimamia utekelezaji wa Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ambayo inalenga katika utendaji wenye matokeo na tija kwa Umma ili kukidhi mahitaji ya Muundo Mpya wa Sekretarieti za Mikoa. Katika mojawapo ya hatua za kufikia lengo hili, Mkoa umejiwekea mkakati wa kuhakikisha kuwa matumizi ya Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) unatekelezwa kikamilifu katika Sekretarieti ya Mkoa, Hospitali ya Mkoa, Ofisi za Wakuu wa Wilaya na Halmashauri zote za Mkoa wa Tabora kuanzia Mwaka wa Fedha 2008/2009. Mafunzo Maalum ya OPRAS yamekwisha tolewa kwa watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa na Ofisi za Wakuu wa Wilaya na utekelezaji wa OPRAS umeanza katika Ofisi hizo. Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora inao Mkataba wa Huduma kwa Mteja (Client Service Charter) ambao ndio kigezo kikubwa cha utekelezaji wa OPRAS. Hatua hii ni katika kutekeleza marekebisho yaliyofanywa katika Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 ya Mwaka 2002 kwa "Amendment" Na.18 ya Mwaka 2007 yanayozingatia matokeo katika utendaji wa kazi na Mpango wa Maboresho ya Utumishi wa Umma Awamu ya II ulioanza mwaka 2008 – 2012. Aidha Sekretarieti ya Mkoa ilikwishafanya Mapitio (Review) ya Mpango Mkakati (Strategic Plan) ya mwaka 2009/2010 hadi 2011/2012 na kuandaa Mpango Mkakati wa mwaka 2010/2011 hadi mwaka 2012/2013. Kwa mwaka 2010/2011 Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora imetenga Tshs.61.5 milioni kwa ajili ya kuwapatia Mafunzo Watumishi wake. Aidha, ili kuhakikisha kwamba kazi zinafanywa kwa kuzingatia matokeo, Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora imepanga ratiba ya Maafisa wake kwenda kuratibu utekelezaji wa shughuli za Serikali katika Halmashauri kila Robo Mwaka.
24.1 Changamoto: Changamoto katika eneo hili ni pamoja na upungufu wa watumishi hasa katika Sekta ya Afya, Elimu na Uzalishaji Mali kutokana na wataalam wengi kutopenda kufanya kazi Mkoa wa Tabora kwa kisingizio cha mazingira magumu.
24.2 Mikakati: Katika kukabiliana na suala la upungufu wa wataalam, waajiri wote Mkoani wamehimizwa kubuni mbinu zitakazowafanya watumishi wavutiwe kuja kufanya kazi Tabora ikiwemo kuwapatia nyumba za kuishi, kuwapa mishara mizuri, motisha ya mazingira magumu n.k. Mkoa pia unajitahidi kushughulikia uboreshaji wa miundombinu na huduma muhimu za kijamii ili kujenga mazingira bora na yanayoweza kuwa kivutio kwa watumishi. Kuwadhamini watumishi katika Taasisi/Asasi mbalimbali za kifedha ili waweze kupatiwa mikopo ya kuwawezesha kununua vifaa vya nyumbani au vya ujenzi wa nyumba za kuishi. SHUGHULI ZA SERIKALI KATIKA UTAWALA BORA:
Shughuli za Serikali katika Utawala Bora zimeainishwa kama ilivyooneshwa hapa chini:- Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Tabora hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2009: (a) Matukio ya Makosa ya Jinai: Makosa Makubwa ya Jinai. Kwa kipindi cha Mwaka 2008 yaliripotiwa jumla ya Makosa Makubwa ya Jinai 6,239 Kwa kipindi cha Mwaka 2009 yaliripotiwa jumla ya Makosa Makubwa ya Jinai 5,826 Kuna upungufu wa makosa makubwa ya Jinai 413. Upungufu huo ni sawa na asilimia 7.08%.
Makosa Madogo ya Jinai: Kwa kipindi cha Mwaka 2008 yaliripotiwa jumla ya Makosa madogo ya Jinai 9,923. Kwa kipindi cha Mwaka 2009 yaliripotiwa jumla ya Makosa madogo ya Jinai 11,146 Kuna ongezeko la makosa madogo ya Jinai 1,223. Ongezeko hili ni sawa na asilimia 12.97%.
(b) 1 . Makosa ya Usalama Barabarani: (i) Kwa kipindi cha mwaka 2008 yaliripotiwa jumla ya Makosa ya Usalama Barabarani 5,001. (ii) Kwa kipindi cha Mwaka 2009 yaliripotiwa jumla ya Makosa ya Usalama Barabarani 4,676. (iii) Kuna upungufu wa makosa ya Usalama Barabarani 325. Upungufu huo ni sawa na asilimia 6%.
2 . Matukio ya Ajali za Barabarani: Kwa kipindi cha mwaka 2008 ziliripotiwa jumla ya Ajali za Barabarani 573. Kwa kipindi cha mwaka 2009 ziliripotiwa jumla ya Ajali za Barabarani 575. (iii) Kuna ongezeko la Ajali za Barabarani 02. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 0.34%.
Matukio ya Ajali za Barabarani zilizosababisha Vifo. Kwa kipindi cha mwaka 2008 ziliripotiwa jumla ya Ajali za Barabarani zilizosababisha vifo 67. Kwa kipindi cha mwaka 2009 ziliripotiwa jumla ya Ajali za Barabarani zilizosababisha vifo 69. Kuna ongezeko la Ajali za Barabarani zilizosababisha vifo 02. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 3%.
Idadi ya Watu Waliokufa kwa Ajali za Barabarani. Kwa kipindi cha mwaka 2009 jumla ya watu waliokufa kwa Ajali za Barabarani ni 91. Kwa kipindi cha mwaka 2008 jumla ya watu waliokufa kwa Ajali za Barabarani ni 76. Kuna ongezeko la watu 15 waliokufa kwa Ajali za Barabarani. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 20%.
Idadi wa Watu waliojeruhiwa kwa Ajali za Barabarani. Kwa kipindi cha mwaka 2009 jumla ya watu waliojeruhiwa kwa Ajali za Barabarani ni 613. Kwa kipindi cha mwaka 2008 jumla ya watu waliojeruhiwa kwa Ajali za Barabarani ni 539. Kuna ongezeko la watu 74 waliojeruhiwa kwa ajali za Barabarani. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 14%. Changamoto zilizopo ni kama ifuatavyo: Baadhi ya makampuni binafsi ya ulinzi kwa ajiri ya walinzi wasiowaaminifu na waadilifu ambao pindi wawapo kwenye maeneo yao ya ulinzi/kazi hufanya mawasiliano na wahalifu na kuwasaidia kutekeleza vitendo vya uhalifu kwenye maeneo yao ya kazi. Wananchi hasa wakulima waishio vijijini kutokuwa na mazoea ya kuhifadhi fedha zao benki hasa baada ya kuuza mazao yao na badala yake kupendelea kutembea wakiwa na fedha zao au kuzihifadhi kwenye nyumba zao. Kwenye mikakati ya kukabiliana na uhalifu iko kama ifuatavyo: Jeshi la Polisi Mkoani Tabora limeandaa utaratibu wa kuhakikisha kuwa walinzi wote walioajiriwa kwenye makampuni binafsi ya ulinzi pamoja na Wakurugenzi wao wanachukuliwa alama za vidole na kupelekwa Polisi Makao Makuu Dar es Salaam Kitengo cha Utambulisho (Forensic Bureau) ili kuona kama hawana kumbukumbu za zamani za uhalifu ndipo waendelee na ajira zao kwenye kampuni husika. Kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kwa kutumia sera ya Polisi Jamii/Ulinzi Shirikishi wajenge tabia ya kuhifadhi pesa zao benki pindi wanapouza mazao/mifugo yao kwa lengo la kupunguza matukio ya uporaji/unyanganyi na wizi. |
|
||||||||||||||||||||||||
| Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, S.L.P. 25, TABORA. TEL: 026 - 2604058/2604116, FAX: 026-2604274 | ||