JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
SERIKALI ZA MITAA
 
Serikali za Mitaa [ Nyumbani ] au
 
 
 

UTEKELEZAJI WA MPANGO WA UBORESHAJI WA SERIKALI ZA MITAA (LGRP):

 

Kabla ya kuisha kwa mpango wa uboreshaji wa Serikali za mitaa awamu ya kwanza (LGRPI) Halmashauri za Mkoa wa Tabora zilikuwa zimefikia hatua mbalimbali za uboreshaji wa miundo. Hatua hizo ni kama ifuatavyo:-

•  Tabora Manispaa ilikwisha tekeleza hatua zote 11 za uboreshaji. Hivi sasa inaendelea na utekelezaji wa mpango mkakati.

•  Igunga ilifikia kwenye utekelezaji wa hatua ya Saba. Katika hatua hii Halmashauri ianchambua muundo wa Halmashauri unaofaa.

•  Sikonge ilifikia kwenye utekelezaji wa hatua ya Tano. Hatua hii inahusu uandaaji wa mpango mkakati.

•  Halmashauri ya Wilaya ya Tabora ilifika kwenye utekelezaji wa hatua ya 8. hatua hii inahusu utekelezaji wa mifumo ya mendeleo ya Watumishi ikiwa ni ajira za Watumishi, kupunguza watumishi na Mafunzo kwa Watumishi.

•  Nzega na Urambo zilifikia utekelezaji wa hatua ya 7 ambayo inahusu uchambuzi wa muundo wa halmashauri unaoofaa.

Baada ya Mpango wa Maboresho Awamu ya Kwanza (LGRP I) KUISHA MWEZI Julai, 2008 shughuli hizo zinatakiwa kusimamiwa na mpango wa maboresho awamu ya pili (LGRP II).

 

Mafanikio:

•  Halmashauri zote zinatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia mipango mikakati na malengo ya kuboresha utoaji huduma bora kwa Wananchi.

•  Halmashauri zimeboresha mifumo ya fedha na Utumishi ambao imesaidia katika utunzaji wa vitabu vya fedha, ukusanyaji wa mapato.

•  Kuongezeka kwa usimamizi wa utoaji wa huduma kwa Wananchi kwa kuzingatia Utawala Bora.

•  Kukua kwa kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri.

 

Changamoto:

•  Ufinyu wa Bajeti ya Sekretarieti ya Mkoa unasababisha wataalam wa Mkoa kushindwa kuzifikia Halmashauri zote na kutekeleza majukumu yake.

•  Mawasialiano duni kati ya Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri kutokana na jiografia ya Mkoa.

•  Uchache wa vitendea kazi kama vile gari, kompyuta n.k kunachangia kuzorota kwa utendaji kazi.

•  Upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali katika ofisi ya Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri unachangia kuzorota kwa utekelezaji wa majukumu.

 

22.3 Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri:

Halmashauri za Mkoa wa Tabora hukusanya mapato kwa kutumia vyanzo vyao vya ndani pamoja na fidia ya vyanzo vilivyofutwa. Kwa mwaka wa fedha 2009/2010, Halmashauri zilikisia kukusanya jumla ya Tshs.6,054,061,214/=.

Hadi kufikia Juni, 2010 zilikusanya jumla ya Tshs.6,462,790,967/= ambayo ni sawa na asilimia 106. Kwa nusu mwaka wa fedha 2010/2011, Halmashauri zimekisia kukusanya jumla ya Tshs.6,656,674,664/= kupitia vyanzo vipya na vya zamani. Ongezeko hilo ni dogo kwa kuwa Serikali kuu imepunguza kodi ya ushuru wa mazao kutoka 5% mpaka 3% chanzo hiki cha mapato ambacho ndiyo tegemeo kwa Halmashauri za Mkoa wa Tabora

Soma zaidi kuhusu mada >>

 

 

 
 
 

 

 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
Serikali za Mitaa [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, S.L.P. 25, TABORA. TEL: 026 - 2604058/2604116, FAX: 026-2604274