JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
MIRADI NA PROGRAMU
 
Miradi [ Programu ] [ Nyumbani ] au
 

Hali ya Uchumi na Maendeleo ya Mkoa:

Uchumi wa Mkoa unategemea zaidi kilimo ambacho kinaajiri takriban asilimia 80 ya wakazi wote wa Mkoa huu. Kutoka katika kilimo mazao ya kutosha ya chakula na biashara huzalishwa. Serikali ya Mkoa husaidiana na Sekta Binafsi katika utoaji wa huduma za kiuchumi na za kijamii ili sekta zingine ziweze kujiendesha.

Aidha, mapato ya ufugaji, uvuvi, urinaji asali, uchimbaji madini na shughuli za viwandani ni ajira mbadala zinazochangia katika pato la wakazi wetu.

Pato la Mkoa limekuwa likipanda mwaka hadi mwaka. Mwaka 2005 pato la Mkoa lilikuwa Tshs.685,104,000,000/= na mwaka 2008 pato lilifikia Tshs.932,640,000,000/=. Kutoka mwaka 2005 hadi mwaka 2008 pato liliongezeka kwa Tshs. 247,536,000,000/= sawa na ongezeko la asilimia 36.

Aidha, Wastani wa Pato la Mtu kwa mwaka liliongezeka kutoka Tshs.362,968/= mwaka 2005 hadi Tshs.429,605/= mwaka 2008, tofauti ya Tshs.66,637/=, sawa na ongezeko la asilimia 13.6.

Ili kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato la Mkoa, Serikali ya Mkoa imedhamiria kuendelea na jitihada zake za kutumia kila fursa iliyopo na inayopatikana Mkoani kutekeleza kwa ufanisi programu za kukuza uchumi na kupunguza umaskini wa kipato. Serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na Serikali Kuu, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Sekta Binafsi, Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Wananchi inaendelea kufanya yafuatayo:

•  Kutekeleza Programu zote za Maendeleo zilizomo Mkoani, hususan katika kilimo, ufugaji, uwindaji wa kitalii na urinaji wa asali.

•  Kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuzingatia miongozo, sera za kisekta na Bajeti ya Serikali.

•  Kuendelea kujenga uwezo zaidi wa Sekretarieti ili ziweze kutekeleza majukumu yake ya kuzisaidia Halmashauri, ili ziweze kuinua ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

•  Kuwekeza mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji ndani ya Mkoa wetu kutoka ndani na nje ya Nchi yetu Tanzania.

Kwa mujibu wa hatua zinachokuliwa Mkoani, tuna matumaini ya kukua kwa uchumi wa Mkoa wetu kwa kasi zaidi, ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2025, Malengo ya Milenia, kupitia utekelezaji wa MKUKUTA na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2005.

Baada ya maelezo haya ya utangulizi, ifuatayo ni taarifa ya kina kisekta katika shughuli za maendeleo Mkoani Tabora.

 

 
 
Miradi [ Programu ] [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, S.L.P. 25, TABORA. TEL: 026 - 2604058/2604116, FAX: 026-2604274