JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
JAMII, JINSIA NA WATOTO
 
[ Jamii ] Jinsia [ Watoto ] [ Nyumbani ] au
 
 
 

SEKTA YA USTAWI WA JAMII:

Mkoa unaratibu shughuli za Ustawi wa Jamii kwa watu wenye ulemavu na watoto walio katika mazingira hatarishi na yatima. Aidha, familia zenye matatizo ya kijamii zimekuwa zikiangaliwa kwa ukaribu zaidi.

HUDUMA ZA MAKUNDI MAALUMU:

 

HUDUMA KWA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI/MAGUMU NA YATIMA:

Mkoa una jumla ya watoto 28,770 wanaoishi katika mazingira magumu na yatima. Wilaya iliyoathirika zaidi ni Nzega ambayo ina watoto 22,751 wanaoishi katika mazingira magumu na yatima.

Mkoa unatekeleza Mpango wa Kitaifa wa Huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi na watoto yatima. Mkoa umekwishajenga jumla ya nyumba 5 kwa watoto hao. Aidha, jumla ya watoto 6,874 wamepewa vifaa na sare za shule, fedha taslimu ziligawiwa kwa watoto 289 na mafunzo ya ufundi wa kazi za mikono yalitolewa kwa watoto 261. Pia, ada za shule zililipwa kwa watoto 4,806 na Bima ya Afya kwa watoto 4,020. Watoto 204 waligawiwa vyakula vya aina mbalimbali, watoto 262 wanapatiwa masomo ya MEMKWA na msaada wa kisaikolojia umetolewa kwa watoto 1,872.

 

HUDUMA KWA VITUO VYA KULELEA WATOTO MCHANA:

Mkoa wa Tabora una jumla ya vituo vya kulelea watoto wadogo mchana 11, vyenye jumla ya watoto 427. Vituo hivyo hutoa huduma ya lishe bora ya uji wa Karanga na Maziwa kwa watoto hao. Wazazi huchangia kuendesha Vituo hivyo kwa kulipia ada ya kiasi cha Shs.1,500/= hadi Shs.2,000/= kwa mwezi.

 

HUDUMA KWA FAMILIA ZENYE MATATIZO:

Mkoa wa Tabora una jumla ya familia 900, zenye matatizo ya kifamilia kama vile wajane, wagane, walioachwa na kuacha, wanaotunza watoto yatima na wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU). Familia hizo zinapata huduma za ushauri nasaha, ambapo mafunzo ya ujasiriamali na vifaa vya kazi hutolewa kama vile vyerehani, vyombo vya kupikia,(mama na baba lishe).

 

CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA USTAWI WA JAMII:

•  Kuwepo kwa vituo vichache vya kulelea watoto mchana.

•  Mwamko na uelewa finyu wa wazazi kutopeleka watoto kwenye vituo vya kulelea watoto mchana.

•  Uzembe wa baadhi ya wazazi kutelekeza familia na kuwaacha watoto kuishi mitaani.

•  Ufinyu wa bajeti za kuwezesha kutoa huduma kwa watoto yatima kwa kujitosheleza.

•  Uhaba wa Wataalam wa Sekta ya Ustawi wa Jamii katika Halmashauri hivyo kazi zao hufanywa na Wataalam wa Maendeleo ya Jamii.

 

MIKAKATI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIZO:

•  Wananchi wanahamasishwa kujenga vituo vya kulelea watoto mchana.

•  Elimu inatolewa kwa kuhamasisha wazazi wawapeleke watoto wao kwenye vituo vilivyopo ikiwa ni pamoja na watoto wenye ulemavu.

•  Kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa kupatiwa vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya kuboresha huduma kwa walengwa.

  Soma zaidi kuhusu mada >>

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
[ Jamii ] Jinsia [ Mifugo ] [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, S.L.P. 25, TABORA. TEL: 026 - 2604058/2604116, FAX: 026-2604274