|
||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||
MASUALA MTAMBUKA:UKIMWI: Tangu Serikali ilipotangaza UKIMWI kuwa ni Janga la Kitaifa Mkoa wa Tabora unaendelea kufanya jitihada ya kupambana na janga hili kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Mashirika mbalimbali na Asasi za Kiraia ndani na nje ya Mkoa zinajitoa kwa hali na mali kupambana na janga hili. Baadhi ya wadau hao ni TACAIDS kupitia RFA, UNDP, BENJAMIN WILLIAM MKAPA HIV/AIDS FOUNDATION, EGPAF na MILDMAY INTERNATIONAL. Shughuli zinazoendelea kufanyika ni pamoja na elimu kwa jamii juu ya njia za maambukizi na jinsi ya kujikinga, hamasa juu ya upimaji wa hiari baada ya kupata ushauri nasaha, huduma ya dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI (ARVs). Mkoa pia unahamasisha shughuli za UKIMWI mahali pa kazi.
HALI YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI (VVU): (a) Januari - Desemba, 2005: Jumla ya watu 45,017 walipimwa kwa hiari. Waliokuwa wakipata huduma ya dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARVs) ni 1,182 sawa na asilimia 29. (b) Januari – Desemba, 2006: Jumla ya watu 95,448 walijitokeza kupima kwa hiari: Wanaume - 17,006 Wanawake - 78,442 Watu waliogundulika na VVU/UKIMWI: Jumla ya watu 7,867 waligundulika kuwa na VVU: Wanaume - 1,911 Wanawake - 5,956 Sawa na asilimia 8. Waliokuwa wakipata huduma ya ARVs 1,820 sawa na asilimia 23.1.
Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto: Jumla ya wajawazito 62,193 walipimwa katika Kliniki mbalimbali Mkoani. Waliogundulika na VVU walikuwa 3,970. Sawa na asilimia 8. (c) Januari – Desemba, 2007: Jumla ya watu 241,571 walipima kwa hiari: Wanaume - 101,585 Wanawake - 139,986 Watu waliogundulika na VVU/UKIMWI: Wanaume - 4,267 (4.2%) Wanawake - 6,861 (4.9%) Jumla - 11,128 (4.6%) Maambukizi ya VVU Kutoka kwa Mama Mjamzito Kwenda kwa Mtoto: Jumla ya akina mama wajawazito 66,481 walipima VVU katika Kliniki mbalimbali Mkoani.
Waliogundulika na VVU walikuwa 2,671 sawa na asilimia 4. Waliohudhuria Kliniki za CTC - 9,595 Walio kwenye ARVs - 3,537 Sawa na asilimia 37.
(b) Kampeni ya Upimaji wa VVU kwa Hiari Julai 14, 2007 Hadi Aprili, 30, 2008: Kampeni ya Upimaji wa VVU kwa hiari ilizinduliwa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 14/07/2007. Lengo la Mkoa wa Tabora lilikuwa kupima watu 218,644. Jumla ya watu 264,503 sawa na asilimia 120 walijitokeza kupima kwa hiari na kuufanya Mkoa wa Tabora kuvuka lengo. Watu waliogundulika na VVU: Wanaume - 4,979 (4.4%) Wanawake - 8,201 (5.4%) 13,180 (4.9%)
(c) Kiwango cha Maambukizi ya VVU Hadi Kufikia Mwezi Juni, 2008: Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na "Tanzania HIV/Aids Survey? 2007/2008 kiwango cha maambukizi ya VVU Mkoani Tabora ni asilimia 6.1 ikilinganishwa na utafiti waliofanya mwaka 2003/2004 ambao maambukizi yalikuwa ni asilimia 7.2. Jumla ya watu 61,346 walipimwa: Wanaume - 15,493 Wanawake - 45,853 Waliogundulika na VVU: Wanaume - 998 (6.4%) Wanawake - 2,723 (5.9%) 3,721 6.1%)
Maambukizi ya VVU Toka kwa Mama Kwenda kwa Mtoto Januari – Juni, 2008: Jumla ya akina mama wajawazito 26,273 walipima VVU katika Kliniki mbalimbali Mkoani. Waliogundulika na VVU ni akina mama 1,088 sawa na asilimia 4. Wanaohudhuria Kliniki ya CTC 16,378 Walio kwenye ARV's 5,439, sawa na asilimia 33. Aidha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ikishirikiana na Taasisi ya Benjamini William Mkapa HIV/Aids Foundation inatekeleza Mradi wa ajira ya dharura unaofadhiliwa na Mfuko wa Dunia (Global Fund) katika kupambana na Kifua Kikuu, Ukimwi na Malaria Mkoani Tabora.
MAFANIKIO KATIKA MASUALA YANAYOHUSU UKIMWI: Huduma za chakula na dawa zimetolewa kwa wananchi waishio na VVU/UKIMWI. Vikundi vya watu waishio na VVU/UKIMWI vimeundwa. Watoto Yatima wameweza kupata mahitaji muhimu ya shule mf. Ada, Sare na vifaa vya Shule. Hali ya Maambukizi imeshuka kutoka asilimia 9 kwa Mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 6.1 kwa utafiti wa mwaka 2007/2008. Hii ni kutokana na juhudi za Serikali na wadau mbalimbali kuwapatia wananchi elimu, hamasa juu ya upimaji wa hiari, huduma ya ARVs na lishe kwa wenye VVU, huduma kwa mama wajawazito (PMTCT) na huduma za nyumbani kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (Home Based Care).
CHANGAMOTO:
Ugonjwa wa Ukimwi unasababisha ongezeko kwa idadi ya watoto yatima na waishio katika mazingira magumu. Kukosekana kwa fedha ya kuwasaidia waishio na VVU/UKIMWI kuwa na mitaji ya kuanzisha shughuli za kudumu. Mwamko mdogo wa wafanyakazi kupima kwa hiari na kujua afya zao. Kuchelewa/Kukwama kwa utekelezaji wa shughuli za Ukimwi kwa Asasi kunatokana na ucheleweshaji au kutopewa fedha walizoahidiwa Mfano: RFA haijatoa fedha kwa Asasi 27 ambazo zimepita kwenye mchakato mbalimbali. Mpaka sasa Ugonjwa wa Ukimwi hauna dawa.
MIKAKATI: • Kuwa na Kampeni ya kudumu ya vita dhidi ya Ukimwi na ufuatiliaji wa Huduma kwa watu waishio na VVU/UKIMWI kuanzia ngazi ya Kitongoji. • Kuendelea kutoa hamasa zaidi kwa watumishi wajitokeze kupima Afya zao. • Ukimwi kuwa agenda ya kudumu katika vikao, mikutano yote kuanzia Ngazi ya Kitongoji. • Kushirikisha wadau mbalimbali ili kuweza kuwapatia mitaji na huduma muhimu watu waishio na VVU/UKIMWI ili waweze kuendesha shughuli za kudumu.
MPANGO WA SERIKALI WA KUWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI: Mikopo iliyotolewa SACCOS kupitia CRDB – 483,600,000/= ya awamu ya kwanza ilinufaisha wananchi 310. Mikopo kwa SACCOS 7 kupitia SCCULT – 250,000,000/= kwa awamu ya pili. Kuna Shs.100m/= zipo kwa ajili ya SACCOS za Wilaya ya Urambo SCCULT inaandaa utaratibu wa kuwakopesha wananchi. Mikopo ya fedha za Benki ya CRDB kwa SACCOS Shs.3,871,258,000/=. Mikopo kwa wananchi fedha za Serikali (Mabillioni ya JK) iliyotolewa kupitia Benki ya NMB ni Shs.283,165,000/=. Jumla ya wananchi 260 walikopeshwa fedha hizo. Urejeshaji wa mikopo siyo wa kuridhisha katika Wilaya ya Nzega na Tabora. Viongozi wa matawi hayo ya benki wanafuatilia urejeshwaji wa fedha hizo.
UWEZESHAJI WA WAJASIRIAMALI WADOGO: Katika kipindi cha Mwaka 2005 – 2009, Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Tabora limewawezesha Wajasiriamali kwa kuwapa mafunzo mbalimbali, vitendea kazi viwandani, mikopo, kuandaa na kuwezesha ushiriki wa Maonyesho ya bidhaa mbalimbali yaliyoandaliwa Kifaifa na Kimataifa. |
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
| Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, S.L.P. 25, TABORA. TEL: 026 - 2604058/2604116, FAX: 026-2604274 | ||