JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
MADA KUHUSU ELIMU HAPA ...
 
Elimu < Mada [ Nyumbani ] au
 
 
 

 

ELIMU YA UFUNDI

 

Katika Mkoa wa Tabora kuna jumla ya Vyuo vya Ufundi Stadi vipatavyo 9 ambayo vinatambuliwa na Mamlaka ya Ufundi Stadi nchini VETA.

Vyuo hivi vina uwezo wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa wakati mmoja kwa wanafunzi 640. Vyuo hivyo vinatoa mafunzo katika fani 9 ambazo ni Uashi, Useremala, Umeme, Useketaji, Uungaji Vyuma, Ufundi Magari, Udereva, Ushonaji, Kompyuta, Upishi, Ufundi Bomba.

 

Uandikishaji:

Jumla ya wanafunzi 2,682 wakiwemo wanafunzi wa kike 1,167 na wa kiume 1,515 waliandikishwa katika vyuo hivi kwa kipindi kati ya mwaka 2005 na 2010 kama ilivyooneshwa katika jedwali Na. 41 hapa chini:

Aidha katika kipindi hicho idadi ya wanafunzi 1,258 walihitimu katika fani mbalimbali kupitia vyuo hivyo kama inavyoonesha katika jedwali lifuatalo:

Hali ya uandikishaji imeendelea kushuka mwaka hadi mwaka kutokana na ongezeko la Shule za Sekondari unaotokana na mpango wa MMES na ule wa Shule za Kata. Wahitimu wengi zaidi huchaguliwa kwenda Shule za Sekondari. Hata hivyo ni matarajio ya Mamlaka ya Ufundi Stadi katika Kanda ya Magharibi kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo kutakuwa na mahitaji makubwa ya mafunzo haya kutokana na ongezeko la wahitimu wa kidato cha nne.

Ili kupata mafanikio ya haraka, Serikali itaongeza ajira kwa kupanua shughuli za VETA Kanda ya Magharibi. Kama sehemu ya maandalizi, shughuli zifuatazo zinafanyika:

(a) Kuanisha na kutenga maeneo ya ukubwa wa hekta 30 kwa Wilaya za Igunga na Uyui ambazo hazina Vyuo vya Ufundi Stadi. Maeneo hayo ni kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vya Wilaya kama ilivyo agizwa na kikosi kazi cha uanzishaji wa vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi;

(b) Kusimamia miradi 2 ya upanuzi wa vyuo vya Tabora na Ulyankulu. Miradi hiyo inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) yenye thamani ya jumla ya Tshs. Bilioni 4.2. Ujenzi wake unatazamiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu. Kumalizika kwa miradi hiyo kunatarajiwa kuongeza uandikishaji wa wanafunzi kutoka jumla ya wanafunzi 300 hadi 500 ikiwa ni ongezeko la asilimia 67% ukilinganisha na uwezo wa awali.

Mafunzo ya muda mfupi (short courses) pia yanatarajiwa kuongezeka ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira katika stadi mbalimbali za ufundi na huduma.

Aidha kumalizika kwa miradi hiyo kutaenda sambamba na kuongezeka kwa fani za ufundi zitakazo tolewa na vyuo hivyo.

 

Changamoto:

Utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi umekuwa ukikumbwa na changamoto mbalimbali katika Mkoa wa Tabora. Changamoto hizo ni pamoja na:

 

•  Kutokuwepo Mpango Mahususi wa Ajira Kwa Wahitimu:

Hakuna mpango mahsusi wa kuwasaidia wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi kuwa wajasiliamali kupitia fani zao. Hali hii husababisha Serikali kupoteza raslimali nyingi hasa pale wahitimu wanapojishughulisha na kazi zingine zaidi ya zile walizopatia mafunzo.

 

(ii)Upungufu wa Vifaa vya Kutolea Mafunzo:

Kumekuwepo na upungufu mkubwa wa vifaa vya kufundishia (Training Tools and Equipment) katika Vyuo. Hali hii ni mbaya zaidi katika vyuo visivyo vya serikali hivyo kuleta wasiwasi juu ya ubora wa mafunzo yatolewayo:

 

Mikakati:

Ili kuondoa umaskini katika Jamii za Watanzania, VETA inatambua Mafunzo ya Ufundi Stadi kuwa moja ya nyenzo muhimu. Jamii isiyo na stadi (Skills) za kazi haiwezi kuongeza tija. Kwa kutambua hilo, VETA:

•  Inaandaa Mpango Mahsusi wa ajira kwa wahitimu ikiwa ni pamoja na kusaidia wahitimu kuunda vikundi vya uzalishaji na kuwapatia vitendea kazi vya msingi pindi wamalizapo mafunzo;

•  Serikali kupitia mpango wa “VETA Support” unaotekelezwa na VETA kuongeza ukubwa wa msaada huo kwa vyuo visivyo vya VETA ili kuleta ubora sawa wa mafunzo katika vyuo vyote.

 

Elimu ya Juu na Ufundi:

Uandikishaji wa Elimu ya Juu kwenye Vyuo Vikuu na Vyuo vya Ufundi imeongezeka hadi 1,832 mwaka 2010 kutoka 256 mwaka 2003.

 

TATIZO LA MIMBA

Tatizo la mimba kwa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi katika mkoa wa Tabora linazidi kupungua kutoka wanafunzi 518 mwaka 2007 hadi 244 mwaka 2009. Kupungua kwa tatizo hilo ni kutokana na hatua za kisheria zinazochukuliwa na Serikali katika udhibiti watu wanaojihusisha na vitendo vya kuwapa mamba wanafunzi hao. Pia elimu ya unasihi inayotolewa kwa wanafunzi shuleni. Jedwali lifuatalo linaonesha mchanganuo wa kila Wilaya kwa mwaka 2009:

 

Hatua Mbalimbali Zilizochukuliwa Dhidi ya Wanaowapa Mimba

Wanafunzi :

Hatua zifuatazo zimechukuliwa katika ngazi mbalimbali za Serikali dhidi ya waliowapa Mimba wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari ni kama ifuatavyo:

•  Jumla ya Kesi 18 za wanafunzi wenye mamba zipo Mahakamani, 135 ya kesi za Mimba zipo katika ngazi ya Serikali ya Kata na Vijiji.

Aidha wanaume 91 waliowapa mimba wanafunzi wamekimbia hivyo serikali za vijiji na kata zipo katika mchakato wa kuwatafuta wanaume hao.

 

 

Mikakati ya Kupunguza Tatizo la Kuwapa Mimba Wanafunzi:

• (i) Viongozi ngazi ya Wilaya, Kata, Vijiji na Mkoa wamelifanya kuwa ajenda ya kudumu katika vikao vyote vya Kiserikali.

• (ii) Kamati/Bodi za Shule zimeelimishwa juu ya Majukumu yao na Kutumia sheria dhidi ya wanaume wanaowapa wanafunzi mimba.

• (iii) Elimu ya Unasihi inaendelea kutolewa mashuleni ambapo wanafunzi wanaelimishwa kuhusu madhara ya kupata mimba katika umri mdogo, kukatisha masomo, na maambukizi ya magojwa hatari.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Elimu < Mada [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, S.L.P. 25, TABORA. TEL: 026 - 2604058/2604116, FAX: 026-2604274