JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
ELIMU
 
Elimu [ Nyumbani ] au
 
 
 

SEKTA YA ELIMU

Elimu ya Awali:

Uandikishaji wa Wanafunzi Elimu ya Awali:

Hali ya uandikishaji wanafunzi wa elimu ya awali Mkoani Tabora inazidi kuimarika. Kwa mwaka 2006, Mkoa ulifanikiwa kuandikisha jumla ya wanafunzi 25,453 wa Elimu ya Awali.

Kwa mwaka 2009, Mkoa ulifanikiwa kuandikisha wanafunzi 41,726 sawa na asilimia 67 ya lengo la wanafunzi 62,278 wa Elimu ya Awali kati yao wavulana ni 17,841 na wasichana 19,165

 

Madarasa ya Elimu ya Awali:

Elimu ya Awali Mkoani Tabora inaendelea kuboreka mwaka hadi mwaka. Mwaka 2006 idadi ya vyumba vya madarasa ya Elimu ya Awali ilikuwa 426, mwaka 2007 kulikuwa na vyumba vya madarasa 536, mwaka 2008 idadi ya vyumba vya madarasa ilifikia vyumba 557, mwaka 2009 kulikuwa na vyumba vya madarasa 661.

Elimu ya Msingi:

IDADI YA SHULE ZA MSINGI:

Mwaka 2009 Mkoa ulikuwa na jumla ya Shule za Msingi 714. Hili ni ongezeko la shule 9 zilizokuwepo mwaka 2008 .

Idadi ya Wanafunzi wa Shule za Msingi:

Mkoa wa Tabora ulikuwa na jumla ya wanafunzi 380,385 mwaka 2008 wa Shule za Msingi.

Kwa mwaka 2009, Mkoa una jumla ya wanafunzi wa Shule za Msingi 397,438. Hivyo kuna ongezeko la wanafunzi 17,053, sawa na asilimia 4

•  Uandikishaji wa Darasa la Kwanza 2005 – 2009:

Kwa mwaka 2005 Mkoa ulifanikiwa kuandikisha jumla ya wanafunzi 65,829 wa Darasa la Kwanza. Kati yao wavulana walikuwa ni 27,548 na wasichana walikuwa 31,781 .

Kwa mwaka 2009 Mkoa umefanikiwa kuandikisha jumla ya wanafunzi wadarasa la kwanza 75,367 sawa na asilimia 97.2 wakiwemo wavulana 39,011 na wasichana 36,356

Uandishaji wa Wanafunzi wa Darasa la Kwanza Mwaka 2010:

Mkoa wa Tabora unategemea kuandikisha wanafunzi 79,957 wa miaka 7 kati yao wavulana ni 40,288 na wasichana 39,669. Aidha Mkoa unatarajia kuandikisha wanafunzi 13,948 wa miaka 8-10 ambao hawakuandikishwa mwaka 2008 na 2009. Hivyo Mkoa kwa mwaka 2010 unatarajia kuandisha jumla ya wanafunzi 93,905 wa kuanzia miaka 7 hadi 10.

 

13.2.4 Majengo ya Shule za Msingi na Samani:

•  Vyumba vya Madarasa:

Kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, jumla ya vyumba vya madarasa 560 vimejengwa sawa na ongezeko la asilimia 367 ya lengo la kujenga jumla ya madarasa 157.

Kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, jumla ya nyumba za walimu 422 zimejengwa sawa na ongezeko la asilimia 343 ya lengo la kujenga jumla ya nyumba 123.

Kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, jumla ya matundu ya vyoo 1,936 yamejengwa sawa na ongezeko la asilimia 343 ya lengo la kujenga matundu ya vyoo 194.

Kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, jumla ya madawati 7,048 yametengenezwa sawa na ongezeko la asilimia 69.5 ya lengo la kutengeneza jumla ya madawati 10,148.

Mafanikio haya makubwa yanatokana na mwamko na mwitikio mzuri wa wadau wa elimu.

 

HALI YA TAALUMA KATIKA SHULE ZA MSINGI:

Mkoa wa Tabora umeendelea kuzijengea uwezo Halmashauri za Wilaya kwa kuzishauri na kufuatilia maagizo yanayolenga uboreshaji wa taaluma. Jedwali lifuatalo linaonesha hali ya ufaulu wa Mtihani wa Darasa la VII kuanzia mwaka 2005 hadi 2009.

Kwa miaka Minne mfululizo (2006-2009) Mkoa umefanikiwa kuwapatia nafasi wanafunzi wote waliofaulu na idadi ya watahiniwa imeongezeka mwaka hadi mwaka.

 

IDADI YA WALIMU:

Mkoa wa Tabora ulikuwa na jumla ya Walimu wa Shule za Msingi 4,986 mwaka 2005.

Kwa mwaka 2009, Mkoa ulikuwa na jumla ya Walimu wa Shule za Msingi 5,863, ikiwa ni ongezeko la walimu 877, sawa na mafanikio ya asilimia 15

 

ELIMU YA SEKONDARI:

Katika mwaka 2005 Mkoa ulikuwa na jumla ya Shule za Sekondari 33 za Serikali ikilinganishwa na mwaka 2010 ambapo kuna jumla ya Sekondari 149 za Serikali.

Hivyo kuna ongezeko la Sekondari 116, sawa na asilimia 452. Ongezeko hilo linatokana na mkakati wa Serikali ya Awamu ya Nne ya kuwa na Sekondari kwa kila Kata na mwitikio wa wananchi katika mkakati huo. Mafanikio mengine yaliyopatikana ni kama ifuatavyo:

•  Kusimamia ujenzi wa nyumba za walimu 185 (sawa na asilimia 199) ya lengo la kujenga nyumba 93.

•  Kuajiri jumla ya walimu 869 ikilinganisha na lengo la kuajiri walimu 361.

Mkoa pia una jumla ya Sekondari 15 za binafsi / Mashirika ya Dini hivyo kufanya idadi ya Shule katika Mkoa kuwa 164.

Idadi ya wanafunzi wenye umri wa miaka 14 – 17 waliofaulu imeongezeka kuandikishwa katika Shule za Sekondari kutoka 51.8% mwaka 2005 hadi 100% mwaka 2009.

 

Wanafunzi walioingia Kidato cha I Mwaka 2010

Jumla ya wanafunzi 36,938 (wavulana 19,403 na wasichana 17,535) walifanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2009. Wanafunzi 14,643 waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza Mwaka 2010 (wavulana 9,027 na wasichana 5,616 ) sawa na asilimia 39.6. Wote wamepatiwa nafasi Kidato cha Kwanza (sawa na asilimia 100).

 

Idadi ya Wanafunzi Watakaochaguliwa Kidato Cha V Mwaka 2010:

Mkoa wa Tabora kwa mwaka 2009 ulikuwa na jumla ya Shule 71 za Sekondari za Serikali za Kidato cha IV. Shule zilikuwa na watahiniwa 4,830 Kati ya hao wavulana ni 2,914 na wasichana ni 1,916.

Mkoa unategemea kwamba wanafunzi 826 waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka 2009 kwa daraja la kwanza hadi la tatu watachaguliwa kujiunga kidato cha tano 2010.

Ili kuweza kuwapatia nafasi wanafunzi 826 waliofaulu Mtihani wa Kidato

cha IV na kuchaguliwa kujiunga Kidato cha V mwaka 2010, jumla ya

vyumba vya madarasa 23, hosteli 8, matundu ya vyoo 41 na madawati

826 yanahitajika ambavyo kwa ujumla vinagharimu kiasi cha Tshs.621,040,000/=.

 

Changamoto:

Kutokana na jedwali lifuatalo, kuna upungufu kama ifuatavyo: vyumba vya madarasa 23, hosteli 16, matundu ya vyoo 42 na madawati 1,003.

Mkakati:

Katika kukabiliana na upungufu huo, Tshs.1.869 billion zinahitajika. Halmashauri za Mkoa wa Tabora zimejipanga kukusanya fedha kutoka kwenye vyanzo vifuatavyo:

•  Serikali Kuu (CDG)

•  Halmashauri

•  TASAF

•  RESOLUTE TANZANIA LIMITED (GOLDEN PRIDE PROJECT)

•  UBALOZI WA JAPAN

•  WADAU WENGINE

Mafanikio ya Ubora wa Elimu ya Msingi na Sekondari:

Kwa upande wa ubora wa mahudhurio ya kila siku darasani kwa wanafunzi, Mkoa umefanikiwa kupandisha kiwango cha mahudhurio na kufikia asilimia 87 mwaka 2009.

Aidha idadi ya wanafunzi wanaomaliza Darasa la Nne imefikia asilimia 74.2 mwaka 2009. Mkoa pia umeweza kuongeza idadi ya wanafunzi wanaomaliza Elimu ya Msingi na kufikia asilimia 68.7 mwaka 2009 ikilinganishwa na asilimia 62 mwaka 2003.

Kwa mwaka 2009 hali ya ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu katika mtihani wa kumaliza kidato cha nne imefikia asilimia 17. Mkoa pia umeweza kuongeza idadi ya Walimu hodari wa Sekondari na Msingi na kufikia asilimia 59.5 mwaka 2009.


13.3.2 Matatizo ya Walimu Mkoani:

•  Upungufu mkubwa wa nyumba za walimu

•  Baadhi ya walimu kutokupandishwa/kucheleweshwa

Kupandishwa madaraja/vyeo.

•  Upungufu mkubwa wa maabara, maktaba, na vifaa vya

kufundishia.

•  Mazingira magumu ya kazi kwa kukosekana kwa huduma za

kijamii katika baadhi ya maeneo zilipojengwa shule.

 

Jinsi Mkoa Unavyokabiliana na Matatizo Hayo:

•  Mkoa kwa kutumia miongozo, unahamasisha jamii ili iweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa nyumba za walimu. Pia Mkoa unaendelea kuzishauri Halmashauri za Wilaya ili zishirikiane na NGOs,FBOs, Makampuni binafsi na Wahisani mbalimbali katika ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa, maktaba na utoaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

•  Halmashauri za Wilaya kwa kutumia Idara za Huduma kwa Walimu zinaendelea kuwapandisha madaraja/vyeo walimu wanaostahili.

•  Halmashauri za Wilaya zinaendelea kuwatumia walimu wa Shule za Msingi wenye Stashahada za Elimu, pamoja na kuwatumia vijana waliohitimu na kufaulu Kidato cha VI.

•  Ili kupunguza tatitizo la upungufu wa walimu Mkoa,unazishauri Halmashauri za Wilaya kuandaa mazingira mazuri ya kuwapokea walimu wapya, pia kuweka vivutio kwa walimu hao.

•  Halmashauri zinaendelea kuboresha miundombinu mfano barabara, simu, umeme, zahanati na vituo vya afya na maji ili kuwavutia walimu.

•  Mkoa unaendelea kuwashauri walimu kujiunga na SACCOS ili kujenga uwezo wa kukopeshwa fedha ili waweze kununua vyombo vya usafiri.

•  Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya husika zinaendelea kudhibiti matukio ya ujambazi na uonevu unaofanywa na baadhi ya watu kwa walimu.

•  Kwa upande wa madai ya walimu, Serikali imelipa kiasi cha Tsh.841,663,889/26. Aidha kiasi cha Tshs.326,194,741/90 zimekatiwa risti na Halmashauri za Wilaya na kuzirudisha Hazina baada ya kuonekana zimezidi.

Serikali pia imeweza kufanikisha zoezi la ulipaji wa madeni ya walimu wa Shule za Sekondari Mkoni, kwa kulipa kiasi cha Tshs.372,034,379/13 ambazo zilikuwa zinadaiwa na walimu katika madai yao mbalimbali

 

Elimu ya Watu Wazima:

Kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, jumla ya madarasa 4,114 yameanzishwa ilinganishwa na lengo la kuanzishwa kwa madarasa 534.

 

MEMKWA:

Huu ni Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa. Mpango huu ulianza mwaka 2004  na kwa mwaka 2005 kulikuwa na madarasa 536 ikilinganishwa na madarasa 632 mwaka 2009.

Kwa mwaka 2005 Mkoa uliandikisha wanafunzi 7,301 kundi rika la I na la II. K wa mwaka 2009, Mkoa uliandikisha wanafunzi 14,723.

 

ELIMU YA UFUNDI:

Katika Mkoa wa Tabora kuna jumla ya Vyuo vya Ufundi Stadi vipatavyo 9 ambayo vinatambuliwa na Mamlaka ya Ufundi Stadi nchini VETA

Vyuo hivi vina uwezo wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa wakati mmoja kwa wanafunzi 640. Vyuo hivyo vinatoa mafunzo katika fani 9 ambazo ni Uashi, Useremala, Umeme, Useketaji, Uungaji Vyuma, Ufundi Magari, Udereva, Ushonaji, Kompyuta, Upishi, Ufundi Bomba.

 

Uandikishaji:

Jumla ya wanafunzi 2,682 wakiwemo wanafunzi wa kike 1,167 na wa kiume 1,515 waliandikishwa katika vyuo hivi kwa kipindi kati ya mwaka 2005 na 2009

Aidha katika kipindi hicho idadi ya wanafunzi 1,258 walihitimu katika fani mbalimbali kupitia vyuo hivyo

Hali ya uandikishaji imeendelea kushuka mwaka hadi mwaka kutokana na ongezeko la Shule za Sekondari unaotokana na mpango wa MMES na ule wa Shule za Kata. Wahitimu wengi zaidi huchaguliwa kwenda Shule za Sekondari. Hata hivyo ni matarajio ya Mamlaka ya Ufundi Stadi katika Kanda ya Magharibi kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo kutakuwa na mahitaji makubwa ya mafunzo haya kutokana na ongezeko la wahitimu wa kidato cha nne.

Ili kupata mafanikio ya haraka, Serikali itaongeza ajira kwa kupanua shughuli za VETA Kanda ya Magharibi. Kama sehemu ya maandalizi, shughuli zifuatazo zinafanyika:

(a) Kuanisha na kutenga maeneo ya ukubwa wa hekta 30 kwa Wilaya za Igunga na Uyui ambazo hazina Vyuo vya Ufundi Stadi. Maeneo hayo ni kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vya Wilaya kama ilivyo agizwa na kikosi kazi cha uanzishaji wa vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi;

(b) Kusimamia miradi 2 ya upanuzi wa vyuo vya Tabora na Ulyankulu. Miradi hiyo inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) yenye thamani ya jumla ya Tshs. Bilioni 4.2. Ujenzi wake unatazamiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu. Kumalizika kwa miradi hiyo kunatarajiwa kuongeza uandikishaji wa wanafunzi kutoka jumla ya wanafunzi 300 hadi 500 ikiwa ni ongezeko la asilimia 67% ukilinganisha na uwezo wa awali.

Mafunzo ya muda mfupi (short courses) pia yanatarajiwa kuongezeka ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira katika stadi mbalimbali za ufundi na huduma.

Aidha kumalizika kwa miradi hiyo kutaenda sambamba na kuongezeka kwa fani za ufundi zitakazo tolewa na vyuo hivyo.

 

Changamoto:

Utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi umekuwa ukikumbwa na changamoto mbalimbali katika Mkoa wa Tabora. Changamoto hizo ni pamoja na:

 

•  Kutokuwepo Mpango Mahususi wa Ajira Kwa Wahitimu:

Hakuna mpango mahsusi wa kuwasaidia wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi kuwa wajasiliamali kupitia fani zao. Hali hii husababisha Serikali kupoteza raslimali nyingi hasa pale wahitimu wanapojishughulisha na kazi zingine zaidi ya zile walizopatia mafunzo.

 

(ii)Upungufu wa Vifaa vya Kutolea Mafunzo:

Kumekuwepo na upungufu mkubwa wa vifaa vya kufundishia (Training Tools and Equipment) katika Vyuo. Hali hii ni mbaya zaidi katika vyuo visivyo vya serikali hivyo kuleta wasiwasi juu ya ubora wa mafunzo yatolewayo:

 

Mikakati:

Ili kuondoa umaskini katika Jamii za Watanzania, VETA inatambua Mafunzo ya Ufundi Stadi kuwa moja ya nyenzo muhimu. Jamii isiyo na stadi (Skills) za kazi haiwezi kuongeza tija. Kwa kutambua hilo , VETA:

•  Inaandaa Mpango Mahsusi wa ajira kwa wahitimu ikiwa ni pamoja na kusaidia wahitimu kuunda vikundi vya uzalishaji na kuwapatia vitendea kazi vya msingi pindi wamalizapo mafunzo;

•  Serikali kupitia mpango wa “VETA Support” unaotekelezwa na VETA kuongeza ukubwa wa msaada huo kwa vyuo visivyo vya VETA ili kuleta ubora sawa wa mafunzo katika vyuo vyote.

Elimu ya Juu na Ufundi:

Uandikishaji wa katika Elimu ya Juu na Ufundi kwenye Vyuo Vikuu na Vyuo vya Ufundi imeongezeka hadi 1,832 mwaka 2010 kutoka 256 mwaka 2003.

Tatizo la mimba kwa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi katika mkoa wa Tabora linazidi kupungua kutoka wanafunzi 518 mwaka 2007 hadi 244 mwaka 2009. Kupungua kwa tatizo hilo ni kutokana na hatua za kisheria zinazochukuliwa na Serikali katika udhibiti watu wanaojihusisha na vitendo vya kuwapa mamba wanafunzi hao. Pia elimu ya unasihi inayotolewa kwa wanafunzi shuleni. Jedwali lifuatalo linaonesha mchanganuo wa kila Wilaya kwa mwaka 2009:

Hatua Mbalimbali Zilizochukuliwa Dhidi ya Wanaowapa Mimba

Wanafunzi :

Hatua zifuatazo zimechukuliwa katika ngazi mbalimbali za Serikali dhidi ya waliowapa Mimba wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari ni kama ifuatavyo:

•  Jumla ya Kesi 18 za wanafunzi wenye mamba zipo Mahakamani, 135 ya kesi za Mimba zipo katika ngazi ya Serikali ya Kata na Vijiji.

Aidha wanaume 91 waliowapa mimba wanafunzi wamekimbia hivyo serikali za vijiji na kata zipo katika mchakato wa kuwatafuta wanaume hao.

 

Mikakati ya Kupunguza Tatizo la Kuwapa Mimba Wanafunzi:

• (i) Viongozi ngazi ya Wilaya, Kata, Vijiji na Mkoa wamelifanya kuwa ajenda ya kudumu katika vikao vyote vya Kiserikali.

• (ii) Kamati/Bodi za Shule zimeelimishwa juu ya Majukumu yao na Kutumia sheria dhidi ya wanaume wanaowapa wanafunzi mimba.

• (iii) Elimu ya Unasihi inaendelea kutolewa mashuleni ambapo wanafunzi wanaelimishwa kuhusu madhara ya kupata mimba katika umri mdogo, kukatisha masomo, na maambukizi ya magojwa hatari.

 

Soma zaidi kuhusu mada >>
         
 
Elimu [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, S.L.P. 25, TABORA. TEL: 026 - 2604058/2604116, FAX: 026-2604274