|
||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||
SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA:
Mkoa unaendeleza Sekta ya Viwanda Biashara na Masoko kwa kushirikisha Sekta Binafsi. Katika utekelezaji, malengo yafuatayo ya Sekta hii yamefanyika: 6.1 Utoaji wa Leseni za Biashara:Hali ya Biashara katika Mkoa wa Tabora: Biashara katika Mkoa imekua zaidi ya mara mbili na nusu katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2005 hadi 2010. Kumekuwa na ongezeko la Jasiriamali ndogo na za kati zinazojishughulisha na biashara za aina mbali mbali. Katika kipindi cha 2005 – Juni 2010 Mkoa umetoa jumla ya leseni za biashara 5,780 kwa Jasiriamali zinazojishughulisha na aina mbalimbali za biashara, ambapo leseni 875 zilizotolewa katika kipindi cha 2005/2006 na leseni 1,010 zilizotolewa 2006/07, leseni 1,000 kwa kipindi cha 2008/09 na leseni 1,230 kwa kipindi cha 2009/10. Katika kipindi cha 2005 – 2009 Mkoa umetoa jumla ya leseni biashara ya usafirishaji wa abiria 559. Kwa upande wa biashara ya usafirishaji mizigo, Mkoa umetoa leseni za usafirishaji abiria 220 kati kipindi cha Agosti 2008 hadi Desemba 2009. Leseni hii zilizokuwa zinajulikana kama TLA zilikuwa zimefutwa na zimeanza kutolewa upya na SUMATRA hapo Agosti 2008. Ongezeko la wasafirishaji kutumia njia za barabara kumetokana na kuboreshwa kwa barabara za Tabora-Itigi kwa kiwango cha changarawe pia uduni wa huduma za mizigo kwa njia ya Reli kumepelekea wasafirishaji kutumia zaidi barabara.
6.2 Upatikanaji wa Bidhaa:Upatikanaji wa bidhaa mbalimbali Mkoani ni mzuri isipokuwa bei ya bidhaa ni kubwa kutokana na wasafirishaji kuongeza gharama kunakosababishwa na ubovu wa barabara ziingiazo Tabora Mjini pamoja na kupanda mara kwa mara kwa bei ya mafuta ya Dizeli na Petroli. Ongezeko la bei za bidhaa hasa za ujenzi kunaathiri miradi mingi Mkoani Tabora ikiwemo ujenzi wa nyumba, shule na barabara.
Huduma za Mabenki:Mabenki yanayotoa huduma katika Mkoa wa Tabora ni NMB, NBC Ltd, CRDB, Barclays Bank (T) Ltd na Benki ya Posta. Benki ya NMB ina mtandao wake katika Wilaya zote za Mkoa na NBC Ltd, ina matawi Tabora Mjini na Wilaya ya Nzega. CRDB na Benki ya Posta zinatoa huduma katika Manispaa ya Tabora. Benki za NMB, CRDB na NBC zinatoa huduma zote za kibenki ikiwa ni pamoja na mikopo na ATM. (Automatic Teller Machine).
6.4 Viwanda:Mkoa una jumla ya Viwanda vikubwa 2, ambavyo ni New Tabora Textile (T) Ltd NTTTL (chenye uwezo wa kuajiri watu 1,000 lakini kwa sasa kinatoa ajira 360) na Tabora Msitu Products Ltd (imeajiri watu 40). Kiwanda cha Nyuzi cha Tabora (New Tabora Textile Ltd) kilifungwa tarehe 05/02/1997 baada ya kushindwa kujiendesha. Kiwanda kilibinafsishwa kwa Kampuni ya New Tabora Textile (T) Ltd na kuanza kazi Aprili 2004. Kwa sasa kiwanda kina jumla ya wafanyakazi 360. Kutokana na kupata umeme na malighafi kidogo ukilinganisha na mahitaji, kiwanda kinafanya kazi chini ya kiwango chake. Inatazamiwa kuwa Kiwanda kitakapofanya kazi kikamilifu, kila siku kitatumia pamba Kilo 23,200. Nchi zinazonunua nyuzi toka New Tabora Textile ni Uturuki, Ureno, Italia, Columbia na China. Mkoa unazo jumla ya Jineri 2 za kuchambua Pamba. Jineri ya Manonga iliyopo Choma Chankola Wilaya ya Igunga ni mbovu kwa zaidi ya Miaka 10. Hata hivyo kwa sasa imepata Mwekezaji. Jineri ya Verian iliyopo Igunga inafanya kazi. Kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la Alizeti Mkoani Tabora, mashine za kusindika zao hilo zimeanzishwa kama ifuatavyo: Manispaa ya Tabora – 6 Urambo – 4 Uyui – 8 Sikonge – 6 Nzega – 7 JUMLA – 31
Pia Mkoa una viwanda vidogo zaidi ya 450 vya upasuaji mbao, kukoboa na kusaga nafaka, ufundi bati na uhunzi. Kila kiwanda kimeajiri kati ya watu 5 – 8.
Mafanikio ya Sekta ya Viwanda na Biashara:Katika kipindi cha 2005 – Juni 2010 Mkoa wa Tabora umekuwa na mafanikio yafuatayo: Kumekuwa na ongezeko la Viwanda vidogo toka 120 Mwaka 2005 hadi 450 Mwaka 2010. Jumla ya Ajira 3,352 zimezalishwa na Wajasiriamali wa Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo Mkoani Tabora.
Changamoto: Uduni na ukosefu wa Miundombinu inayounganisha wazalishaji na masoko ya ndani na nje. Hii ni pamoja na ukosefu wa barabara nzuri zinazounganisha Wilaya na Vijiji, kuwa na Uwanja wa mdogo wa Ndege usioweza kutumika kwa Ndege za mizigo. Ukosefu wa miundombinu bora ya Maji na hivyo ni vigumu kwa Wawekezaji kuwekeza Tabora hasa kwa Viwanda vikubwa vinavyohitaji maji mengi kama cha Soda. Huduma duni za Reli ya Kati ambayo ni tegemeo kubwa kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa na malighafi. Kupanda mara kwa mara kwa bei ya mafuta ya dizeli na petroli.
Mikakati ya Kupambana na Changamoto:Serikali ngazi ya Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri na Wadau wengine wa Maendeleo imeanza kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto hizi kama ifuatavyo: Katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa mitaji kwa Wajasiriamali, Mkoa unawaelimisha wananchi kutumia ya kuwepo kwa mfuko wa pembejeo ili kujipatia mkopo ya matrekata na pembejeo na hivyo kuweza kufanya kilimo cha kibiashara na kuweza kutekeleza azma ya Serikali ya kutekeleza "Kilimo Kwanza? Mkoa unawahamasisha wananchi kutumia fursa ya Mpango wa Kitaifa wa kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kupitia Benki ya TIB, Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ili kuweza kupata mikopo ya kununulia mashine na kuweza kuanzisha viwanda vya kusindika na kuongeza thamani mazao ya kilimo kama alizeti, mahindi, karanga na mihogo. Aidha Mkoa unawahamasisha wananchi kuunda vikundi ya ushirika pamoja na Vyama vya Kuweka Akiba na Kukopa (SACCOS) ili kupunguza tatizo la ukosefu wa mitaji. Mkoa unatarajia kuutumia Mkakati wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) ili kusaidia wananchi kupata hati rasmi za umiliki wa Ardhi, Nyumba na Mali zingine ili kuweza kuvitumia kukopa katika Benki. Serikali ngazi ya Mkoa itaendelea kudumisha ushirikiano na Baraza la Biashara la Mkoa, Chama cha Wenye Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) pamoja na Asasi zisizo za kiserikali ili kuijengea uwezo Sekta Binafsi.
UWEKEZAJI:
Mkoa wa Tabora unachukua hatua madhubuti katika kukuza uwekezaji kwa lengo la kuongeza ajira, kukuza pato la Mkoa na kuboresha maisha ya jamii. Maandalizi ya kuvutia Wawekezaji yaliyokwishafanyika ni kama ifuatavyo: (i) Mkoa umekamilisha mchakato wa kuainisha maeneo ya ardhi kwa ajili ya kupimwa na kupatiwa hati miliki. Maeneo hayo ni: Mashamba ya Kilimo cha Kibiashara Kilimo cha Umwagiliaji Ranchi Maeneo Maalum kwa ajili ya Viwanda Vikubwa (Industrial Estates) Ardhi kwa ajili ya nyumba za biashara kama Hoteli. Aidha Mkoa unaandaa Andiko la Kutangaza Fursa za Wewekezaji zilizopo na mazingira ya kufanya biashara. Miongoni mwa maen eo yaliyoainishwa kwa ajili ya uwekezaji wa Viwanda katika Manispaa ya Tabora ni Malolo lenye ukuwa wa km.1 na barabara ya Kilimatinde lenye ukubwa wa km.1.7. Maeneo yote haya yana huduma za umeme, barabara na reli. Pia, hayako mbali na Uwanja wa Ndege wa Tabora. Aidha, Mkoa umeainisha eneo lenye ukubwa wa ekari 106,240 (Hekta 42,496) kwa ajili ya Wawekezaji katika ufugaji wa kibiashara. Eneo hili la Kisasiga liko katika Wilaya ya Nzega ambapo jumla ya ng'ombe 12,140 wanaweza kufugwa. Ng'ombe mmoja wa nyama atahitaji eneo lenye wastani wa ukubwa wa hekta 3.5 kwa mwaka. Eneo hili ni fursa muhimu hususan kwa wafugaji wa ng'ombe wa nyama kwa kuzingatia kwamba liko karibu na kiwanda cha nyama cha Shinyanga. (ii) Mkoa unaendelea kuboresha Tovuti yake ( www.rastabora.go.tz ) kwa lengo la kurahisisha teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambapo vivutio vyote vya Uwekezaji vya Mkoa vitawekwa. (iii) Mkoa unaandaa Kongamano la Wawekezaji (Investor's Forum) kwa ajili ya kuvutia uwekezaji. (iv) Kwa kushirikiana na Baraza la Taifa laBiashara (TNBC)*, TCCIA*,CTI* na TIC*, Mkoa unaandaa warsha kwa ajili kuwaelimisha Wadau na Wananchi kwa ujumla namna ya kufaidika na Mikataba ya Kiubia ya Kiuchumi (Economic Partnership Agreements – EPA ) pamoja na Mpango wa AGOA* . Tayari Mkoa umekwisha andaa Baraza la Biashara la Mkoa na Mabaraza ya Biashara ya kila Wilaya.
TNBC - " Tanzania National Business Council? TCCIA - " Tanzania Chamber of Commerce, Industries and Agriculture? CTI - "Confederation of Tanzania Industries? AGOA - "Africa Growth and Opportunity Act? (v) Aidha, Mkoa utatumia fursa zilizopatikana katika Mkutano wa SULLIVAN wa Juni, 2008 Mjini Arusha ambao una fursa nyingi za kupata wawekezaji kwa ajili ya Sekta ya Utalii. Soma zaidi kuhusu mada >>
|
|
||||||||||||||||||||||||
| Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, S.L.P. 25, TABORA. TEL: 026 - 2604058/2604116, FAX: 026-2604274 | ||