|
||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||
SEKTA YA BARABARA:SEKTA YA BARABARA: Mtandao wa barabara Mkoani Tabora una jumla ya Km 5,588.31; Barabara Kuu Km 964.5, Barabara za Mkoa Km 744.2, Barabara za Wilaya km 1,516.96, na Barabara za Vijiji ni Km 2,362.69. Katika mtandao mzima wa Barabara Kuu na za Mkoa ni kilometa 158.6 tu ndizo zenye lami na zilizobaki ni za changarawe na udongo.
8.1 Matengenezo ya Barabara Mwaka 2009/2010 i) Barabara Kuu Katika mwaka wa fedha 2009/2010 jumla ya kilometa 1,246.8 za Barabara Kuu zilitengewa jumla ya Shilingi 3,164.142 milioni kwa ajili ya matengenezo ya kawaida, muda maalum, sehemu korofi na madaraja. Baadhi ya barabara zimepangiwa kupata matengenezo ya kawaida katika mizunguko miwili kwa mwaka, hivyo kusababisha ongezeko la urefu wa matengenezo ukilinganisha na urefu wa mtandao. Hadi kufikia mwisho wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2009/2010 jumla ya kilometa 185.5 za barabara na madaraja mawili na makalavati 70 yamefanyiwa matengenezo kwa gharama ya Ths.347.561/= Milioni.
ii) Barabara za Mkoa Katika Mwaka wa fedha 2009/2010 jumla ya kilometa 543.5 za Barabara za Mkoa zimetengewa jumla ya Tshs.1,663.9/= Milioni kwa ajili ya matengenezo ya kawaida, muda maalum, sehemu korofi na madaraja. Urefu wa matengenezo umekuwa pungufu kulinganisha na urefu wa mtandao kutokana na ongezeko la barabara zilizopandishwa daraja baada ya Bajeti ya mwaka kupitishwa, hivyo kutojumuishwa kwenye bajeti hiyo.
Hadi kufikia mwisho wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2009/2010 jumla ya matengenezo ya kilometa 47.5 za barabara, matengenezo ya kawaida ya madaraja 66 na matengenezo makubwa ya daraja moja yamefanyika kwa gharama ya Tshs.371.628 Milioni. Barabara za Wilaya: Jumla ya km1164 sawa na asilimia 85.2 kati ya Km.1,366 ya barabara za Wilaya zimekarabatiwa kawa kipindi cha miaka 5 na zinapitika vizuri. Barabara za Vijiji: Jumla ya km 53.9 sawa na asilimia 7% zimekarabatiwa. Kiwango hiki ni chini ya lengo la kufanya matengenezo hadi kufikia asilimia 75 ifikapo 2009/2010. Hii ni kwa sababu wananchi wengi bado wanaendelea kutegemea Serikali kuwatengenezea barabara pasipo wao kushiriki. Hata hivyo jitihada zinaendelea za kuhamazisha Jamii ili iweze kushiriki katika kufanya shughuli za barabara zilizo ndani ya uwezo wao katika maeneo wanakoishi.
Matengenezo ya Barabara kwa Kutumia Fedha Toka Mfuko wa Maendeleo. Jumla ya Tshs.1,501/= Milioni zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya kilometa 86.5 za Barabara za Mkoa kutoka kwenye Mfuko wa Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2009/10. Hadi kufikia mwisho wa Robo ya Pili ya mwaka wa fedha 2009/10, jumla ya kilometa 19 za barabara zimefanyiwa matengenezo ya ukarabati kwa kiwango cha changarawe. Hata hivyo bado hakuna malipo ambayo yamefanyika na kazi bado zinaendelea. Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2007/08, jumla ya shilingi 1,874/= Milioni ziliidhinishwa kwa ajili ya ujenzi na usimamizi wa kilometa 3 za barabara ya Tabora – Urambo (sehemu ya mjini) kwa kiwango cha lami. Kazi hiyo ilipangwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti 2009, hata hivyo ilikamilika katikati ya mwezi Novemba 2009 kwa gharama ya shillingi 1,764/= Milioni ambayo ni asilimia 94.2 ya gharama za mradi huo. Fedha iliyobaki italipwa baada ya kuridhika na uimara wa barabara hiyo baada ya kipindi cha matarajio (Defect Liability Period) kumalizika. 8.2 Utekelezaji wa Miradi ya Kitaifa: Barabara ya Mpanda – Koga – Tabora (359) Mradi huu unahusisha upembuzi yakinifu wa kina, tathmini ya athari za kimazingira na kijamii na uandaaji wa nyaraka za zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami. Mradi unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania. Mkataba kati ya Wakala wa Barabara na Mhandisi Mshauri M/S COWI A/S kwa kushirikiana na M/s Cowi Tanzania ulisainiwa tarehe 08/06/2009. Gharama za mradi ni shilingi za kitanzania 1,151,953,642.00 na DKK 4,288,900.
Barabara ya Nzega – Tabora (116 km) Mradi huu unahusiha usanifu wa kina, tathimini ya athari za kimazingira na kijamiii na uandaaji wa nyaraka za zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami. Mradi unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania. Mkataba kati ya Wakala wa Barabara na Mhandisi Mshauri M/s COWI A/S kwa kushirikiana na M/S COWI Tanzania ulisainiwa tarehe 12/12/2009. Gharama za mradi ni Tshs.1.2. bilioni.
Barabara ya Tabora – Nyahua – Chaya (165.5 km) Mradi unahusisha uboreshaji wa taarifa ya usanifu wa kina na uaandaaji wa nyaraka za zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami. Mradi unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania. Mkataba wa mradi ulisainiwa kati ya TANROADS na mhandisi mshauri M/s Crown-Tech tarehe 7 Septemba, 2009 kwa kipindi cha miezi sita (6). Gharama ya mradi ni Tshs. 673,375,000/=.
Barabara ya Kaliua – Malagarasi River – Ilunde (156 km) Mradi huu unahusisha usanifu wa kina, tathimini ya athari za kimazingira na kijamii na uandaaji wa nyaraka za zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami. Mradi unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania. Mkataba kati ya wakala wa Barabara na Mhandisi Mshauri M/S Crown – Tech ulisainiwa mwaka 2007. Gharama za mradi ni Tshs.582 millioni. Kazi ya usanifu wa kina imekamilika mwaka 2008. Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo.
Barabara ya Tabora – Urambo (126 km ) Kazi ya usanifu wa barabara yote kilometa 126 ilikamilika 2007. Kutokana na ufinyu wa bajeti kwa ajili ya ujenzi imeonekana ni vema nyaraka za zabuni zikagawanywa katika sehemu mbili ili kuanza na Kandarasi ya ujenzi wa sehemu ya Tabora – Ndono yenye urefu wa kilometa 42. Mkataba kati ya Wakala wa Barabara na handishi M/s Makconsult kwa ajili ya ugawanyaji wa nyaraka za zabuni ulisainiwa tarehe 07/01/2010 kwa gharama ya Tshs.57,800,000/=.
CHANGAMOTO TUNAZOKABILIANA NAZO:(i) Bajeti isiyokidhi mahitaji halisi ya matengenezo na ukarabati wa barabara pamoja na madaraja. Pia, mara nyingi fedha hutolewa wakati wa msimu wa mvua au unapokaribia. Hali hii husababisha kiasi kikubwa cha fedha kisiweze kutumika katika kipindi hicho. (ii) Uharibifu na wizi wa samani za barabara, hali ambayo inatishia usalama wa watumiaji wa barabara, mali zao, miundombinu pamoja na kuongeza gharama zisizo za lazima kwa serikali wakati wa kurekebisha uharibifu ambao ungeweza kuepukika (iii) Uhaba wa vyanzo vya maji kwa ajili ya matengenezo ya barabara na madaraja ndani ya Mkoa wetu. (iv) Magari mazito kupitishwa kwenye barabara za Mkoa na hivyo kusababisha makalavati na barabara kuharibika haraka kuliko inavyotazamiwa baada ya kufanyiwa matengenezo. (v) Wakandarasi kukatazwa kuchukua changarawe kwenye baadhi ya sehemu wakati wa utekelezaji wa miradi ya barabara kwa maendeleo ya sehemu husika.Wana Vijiji wanadai malipo ambayo hayamo ndani ya Mikataba. Sehemu za hifadhi ya wanyama na misitu pia matatizo hujitokeza wakati wa kufanyia matengenezo barabara zinazopita ndani ya hifadhi hizo. Halikadhalika wanamazingira wanasema uchimbaji changarawe na ukataji miti iliyo kandokando ya barabara pale upanuzi wa barabara unapohitajika ni kuharibu mazingira na hivyo ni matatizo. (vi) Udhaifu katika kutekeleza kazi kunakosababishwa na ukosefu wa mitaji, uhaba wa wataalam, vitendea kazi, pamoja na uzoefu sahihi miongoni mwa Makandarasi. (vii) Kutoboresha mara kwa mara stadi za wataalam wanaowasimamia Makandarasi.
MIKAKATI YA KUKABILI CHANGAMOTO: Kwa vile tatizo kubwa la fedha za matengenezo ya barabara na madaraja hutolewa kidogo linatokana na ufinyu wa Bajeti, hoja zimetolewa ili pindi mapato ya Serikali yanapoongezeka, fedha zitolewe kulingana na mahitaji na katika muda muafaka ili baadhi ya kazi zianze kutekelezwa kabla ya msimu wa mvua. Kwa kuwa ulinzi shirikishi ni njia inayoweza kunusuru samani za barabara kwani uharibifu mwingi hufanyika kwenye maeneo wanamoishi watu, katika vikao vya Bodi ya Barabara ya Mkoa, tunakumbushana kuwa kamati za ulinzi na usalama za Wilaya na zile za Serikali za Vijiji zihusike moja kwa moja na ulinzi wa samani za barabara katika maeneo yao. Imependekezwa pia kupiga marufuku biashara ya vyuma chakavu ndani ya Mkoa ili kupunguza tatizo la wizi wa vyuma. Ili kupunguza tatizo la maji ya kutumia wakati wa kutekeleza miradi ya barabara Mkoani, fedha zikitolewa mapema na kazi zikatangazwa mapema, kuna uwezekano mkubwa wa kufanyika baadhi ya kazi kabla changarawe hazijapoteza unyevu. Utaratibu huu umeanza kutumika mwaka 2009. Wito unaendelea kutolewa kwa wasafirishaji ili waheshimu alama zinazoonyesha uzito unaoruhusiwa kwenye barabara husika. Hali hii itazifanya barabara zetu zitumike kwa muda mrefu zaidi bila kuharibika mapema baada tu ya kutengenezwa kama ilivyo sasa. Tunatoa wito kwa viongozi wetu wa Kitaifa kujadili suala hili na kulitolea maamuzi ili kuwarahisishia watendaji ngazi za utekelezaji. Pamoja na kwamba Makandarasi wana vyama vyao na kwamba bado tatizo la ukosefu wa mitaji kwa ajili ya kuendesha shughuli za utekelezaji wa kazi za ujenzi lingalipo, inapendekezwa kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kusaidia Makandarasi wazalendo namna ya kupata mitaji ikiwa ni pamoja na kuangalia sheria za mabenki ili zifungue milango itakayowawezesha kupata mikopo kwa urahisi zaidi. |
|
||||||||||||||||||||||||
| Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, S.L.P. 25, TABORA. TEL: 026 - 2604058/2604116, FAX: 026-2604274 | ||