JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
 
     
ARDHI, UPIMAJI NA RAMANI
 
Ardhi [ Upimaji ] [ Ramani ] [ Nyumbani ] au
 
 
 

SEKTA YA ARDHI:

 

Katika kipindi cha kuanzia 2005 hadi 2010, utekelezaji wa shughuli za Sekta ya Ardhi za kutayarisha Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi mijini, kupima viwanja na kuuandaa Hati miliki za Ardhi umekuwa kama ifuatavyo:-

Jumla ya viwanja vipya 16,923 vimebuniwa katika maeneo ya miji Mkoani Tabora katika kipindi cha mwaka 2005/2006 hadi 2009/2010. Aidha, katika kipindi hicho viwanja 8,680 vimepimwa, ambapo viwanja 5,986 vimepimwa katika Makao Makuu ya Wilaya na viwanja 2,694 katika Makao Makuu ya Mkoa. Aidha, jumla ya Hati za muda mrefu za miliki za Ardhi 1,488 zimetayarishwa katika kipindi cha kuanzia 2005/2006 hadi 2009/2010.

Mabaraza ya Ardhi

Mkoa wa Tabora unalo Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya lenye Ofisi zake kwenye jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Baraza hili lilianza kufanya kazi kuanzia mwaka 2005. Aidha, katika kila Wilaya Mkoani Tabora Kata zote zina Mabaraza ya Ardhi ya Kata. Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji yaliyokwisha undwa ni 193 sawa na asilimia 39.5% ya vijiji vyote. Aidha, Mkoa unaendelea kuratibu mabaraza ya Ardhi ya Kata ili kuona yanavyokidhi matakwa ya Sheria ya Utatuzi wa migogoro ya Ardhi Na.2 ya 2002 kuhusu muundo wa mabaraza hayo.

Ingawa Mabaraza ya Ardhi ya vijiji yalianzishwa kama inavyooneshwa katika jedwali hili, wajumbe wake ni wa kuteuliwa kwa miaka mitatu na mjumbe anaweza kuteuliwa tena kipindi chake kikiisha. Kwa hali hiyo Mabaraza ya vijiji 193 tu, sawa na asilimia 35.5 ya vijiji vyote ndiyo yenye wajumbe ambao kipindi chao hakijaisha. Katika mwaka 2010/2011 zoezi la uteuzi mpya wa wajumbe litahimizwa kufanyika.

 

7.2 Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi:

Halmashauri zote katika Mkoa zilikwisha kupewa maelekezo ya kuwezesha Kamati hizo kifedha ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi. Pia, mabaraza yote ya Kata yalikwishapelekewa nakala za Sheria ya Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi ili kuwaongoza wajumbe wa Mabaraza hayo katika utendaji kazi wao.Katika mwaka 2005, Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Tabora lilipokea migogoro ya Ardhi 64 na mpaka sasa migogoro yote imekwishatolewa uamuzi. Mwaka 2006 lilipokea migogoro 52 na mpaka sasa yote imekwishatolewa uamuzi. Mwaka 2007 lilipokea migogoro 57, migogoro 54 imekwishatolewa uamuzi mpaka sasa na miwili (2) bado haijatolewa uamuzi. Mwaka 2008 lilipokea migogoro 83, migogoro 64 imekwishatolewa uamuzi na 19 bado haijatolewa uamuzi. Mwaka 2009 limepokea migogoro 126, migogoro 67 imekwishatolewa uamuzi na 59 bado haijatolewa uamuzi. Aidha, Baraza hili katika mwaka 2005 lilipokea Rufaa moja kutoka Mabaraza ya Kata. Rufaa hiyo ilisikilizwa na kutolewa uamuzi. Mwaka 2006 zilipokelewa Rufaa 12 na zote zimekwishatolewa uamuzi. Mwaka 2007 Baraza lilipokea rufaa 26 na zote zimekwishatolewa uamuzi. Mwaka 2008 lilipokea Rufaa 49 na zote zimekwisha tolewa uamuzi. Mwaka 2009 zimepokelewa jumla ya Rufaa 80 kati ya hizo Rufaa 42 zimesikilizwa na kutolewa uamuzi na 38 bado zinaendelea kusikilizwa.

Pia, mwaka 2005 Baraza lilipeleka mgogoro 1 kwenye Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kwa ajili ya Rufaa. Mwaka 2006 lilipeleka migogoro 9, mwaka 2007 lilipeleka migogoro 13. Mwaka 2008 Baraza lilipeleka migogoro 28 na mwaka 2009 limepeleka migogoro 21.

Aidha kwa kipindi cha mwaka wa fedha kuanzia Julai, 2009 mpaka sasa Baraza limepokea jumla ya migogoro 42 kati ya hiyo migogoro 21 imetolewa uamuzi na migogoro 21 bado inaendelea kusikilizwa. Rufaa zilizopokelewa toka kwenye Mabaraza ya Kata ni 30 kati ya hizo 22 zimetolewa uamuzi na 8 bado zinaendelea kusikilizwa. Kesi zilizokatiwa Rufaa kwenda Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ni 12.

Jumla ya kesi zote zilizopokelewa tangu Baraza lianze kazi mwaka 2005 mpaka sasa ni 382, zilizotolewa uamuzi ni 301 na ambazo hazijatolewa uamuzi ni 81.

Pia, jumla ya Rufaa zilizopokelewa tangu mwaka 2005 mpaka sasa ni 168, ambazo zimetolewa uamuzi ni 130 na ambazo hazijatolewa uamuzi ni 38. Aidha, kesi zilizokatiwa Rufaa kwenda Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi tangu mwaka 2005 mpaka sasa ni 72.

 

CHANGAMOTO:

•  Utekelezaji wa shughuli za Sekta hii ikiwa ni pamoja na utatuzi wa migogoro ya Ardhi unakabiliwa na uhaba mkubwa wa wataalam wa fani mbalimbali za Sekta ya Ardhi katika Halmashauri. Uhaba upo katika fani za Mipango Miji, Upimaji Ardhi, Usimamizi wa Ardhi na Uthamini.

•  Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi inatayarishwa kwa kasi ndogo mno kutokana na uhaba wa fedha za kutekeleza shughuli hiyo.

Soma zaidi kuhusu mada >>

 

 
         
 
Ardhi [ Upimaji ] [ Ramani ] [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, S.L.P. 25, TABORA. TEL: 026 - 2604058/2604116, FAX: 026-2604274